Friday, October 14, 2016


 MSHAMBULIAJI wa Yanga,  Saimon Msuva , Jumatano ya Juma hili alifunga bao moja kwenye ushindi wa Yanga wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.
Watunzaji wa kumbukumbu wanasema goli hilo lilimfanya Msuva afikishe mabao 50 katika mechi 164 alizoichezea Yanga kwenye mashindano yote tangu ajiunge nayo Mwaka 2012 akitokea Moro United.
Hata hivyo watu wengi walitamani kujua, katika mabao hayo 50, ni lipi Msuva anaamini ni bora zaidi kwake kuwahi kulifunga?
“Goli langu bora hadi sasa katika magoli 50 toka nianze kuitumikia Yanga ni lile nilowafunga Ruvu mwaka juzi. Nilifunga kwa kichwa (diving header), nalifananisha na goli la Robin van Persie alilofunga kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil dhidi ya Hispania,”
alisema Saimon Happygod Msuva.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video