YAWEZEKANA ni kosa kubwa lililofanywa na uongozi wa Yanga kuachana na Pluijm pia yaweza kuwa ni jambo la heri na la maendeleo kwa kumuajiri kocha mpya Mzambia George Lwandamina.
Tusiishie kuubeza uongozi wetu kwa mabadiliko haya, inatupaswa kujiuliza uwezo wa huyu
anayekuja kumbadili Pluijm!Je ana vigezo vya kumfanya awe bora kumzidi babu mpaka kuushawishi uongozi wetu?ukipitia wasifu wake utaona pia viongozi wa Yanga wanapaswa kupewa pongezi, ni dhahiri wamevuja jasho kwa kuipigania saini ya Lwandamina ambaye vilabu vikubwa barani Afrika vilikuwa vikimwania.
Kabla ya kubeza mabadiliko haya tenga muda wako kumfahamu Lwandamina ni nani, kabla ya kumlilia Pluijm weka akiba ya furaha itakayomuelezea Lwandamina kwa siku za usoni kutokana na mafanikio yake. Uongozi huu ndio uliomleta na kumtambulisha kwetu Hans Van Pluijm pia ni uongozi huu huu unamleta kocha bora Mzambia Lwandamina. Tuache uoga.
Kinacho takiwa ni kumshukuru babu Hans Van Pluijm kwa alipo tufikisha , pia kumkaribisha kocha mpya! Imani yangu viongozi wanajuwa zaidi kuliko sisi ambao mara zote tunasubiri taarifa, tuombee mabadiliko haya yawe yenye tija kwa mustakabali wa klabu yetu, yatupasa tuungane na kumpa ushirikiano mwalimu mpya huo ndo wajibu wetu.
Acha tutokwe chozi la huzuni tukimuaga Pluijm pia chozi hilo hilo liwe ishara ya ushindi tunapomkaribisha Lwandamina.
Instagram : hissansalum
0 comments:
Post a Comment