Baada ya kuibuka tetesi kuwa amateuliwa kuwa kocha msaidizi wa Yanga, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema hajafanya mazungumzo yoyote na klabu hiyo.
Mkwasa amesema kuwa taarifa hizo zimemstua sana kutokana na ukweli kwamba kwa sasa yeye ni kocha wa timu ya taifa.
” Nashangazwa na taarifa hizo zinazosema naenda Yanga kuwa kocha msaidizi. Nina mkataba wa kuifundisha timu ya Taifa. Hakijabidilika kitu. Toka kocha mkuu hadi kocha msaidizi itakuwa ni jambo la ajabu sana.” Mkwasa amesema.
Kabla ya kukabidhiwa majukumu ya kuinoa Taifa Stars, Mkwasa alikuwa kocha msaidizi wa Yanga chini ya kocha aliyebwaga manyanga, Hans Van Der Pluijm.
0 comments:
Post a Comment