Meneja wa Yanga Hafidhi Saleh akanusha kujiuzulu nafasi yake kwenye klabu hiyo kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari hapo awali kufuatia taarifa za kujiuzulu aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm.
Hafidhi amesema kuwa yeye bado ni meneja halali wa klabu hiyo na kuwasihi wana Yanga kupuunza taarifa hizo ambazo ameziita ni za kuzushi.
" Bado mimi naendelea na kazi yangu kama meneja wa timu na habari zinazoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kwamba nimejiuzulu ni za uongo. "
Hafidhi anaungana na Juma Mwambusi ambaye anakaimu nafasi ya kocha mkuu hivi sasa sambamba na Kocha wa Makipa Juma Pondamali kuiongoza timu hiyo katika michezo iliyobaki ya mzunguko wa kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment