Wednesday, October 12, 2016



Na Abdallah Salehe-Mdau wa MPENJA SPORTS

MBEYA CITY leo kuanzia saa 10:30 Jioni wanaikaribisha Simba SC katika mechi ya Ligi Kuu ya Kandanda Tanzania Bara Uwanjani Sokoine, Mbeya.
Kwa mtazamo wangu, Nafikiri mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuangalia ubora wa vikosi vyote na nafasi za timu hizo kwenye msimamo wa Ligi kuu huenda ikaongeza  changamoto zaidi ya mchezo huo.
Mbeya City inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikijikusanyia pointi 12 kwa kucheza mechi 8 ni wazi itaingia Dimbani kusaka alama tatu muhimu ili kuendelea kujiweka mazingira mazuri
Mbeya City wanaotumia sana mfumo wa 4-4-2 angle wakiucheza katika wide formation, kiufundi wanaonekana kuimarika sana katika pattens zao za uchezaji. Ni wazuri sana kwa kujenga mashambulizi ya kasi kutokea pembeni huku muunganiko wao ukionekana kuwa mzuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
John kabanda na Hassan Mwasapili wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuzuia na kutoa msaada kwa mawinga wao Geofrey Mlawa na Joseph Mahundi ili kujenga mashambulizi ya kutokea pembeni.
Kwenye idara ya kiungo, Mbeya City watatakiwa kuwa makini sana na aina ya uchezaji wa viungo wa simba,bila shaka Nahodha wao, kenny Ally ataendelea kusimama vyema kucheza defensive midfielder akitakiwa kuilinda safu ya ulinzi kwa kufanya ya kupokonya mipira na kuwatawanya viungo wa Simba na kumfanya Raphael Daud kuwa kiungo huru wa kuchezesha timu ikizingatiwa huyu ndiye key player anayeiunganisha timu na kuubeba mfumo wa uchezaji.
Idara ya ushambuliaji ya Mbeya City ni wazi itatakiwa kuwa na mabadiliko kidogo ya uchezaji kwa kuzingatia idara ya ulinzi ya Simba ambayo sio nzuri sana kwa kucheza high balls, pia watatakiwa kuongeza umakini katika kutumia nafasi chache zitazotengenezw.
Idara ya ulinzi ya Mbeya City itatakiwa kuwa compact na kucheza kwa umakini mkubwa kutokana na aina ya ushambuliaji wa timu ya Simba huku watu kama Shiza Kichuya na Ibrahim Ajib wakiwapa special attention.
Kwa upande wa timu ya Simba ambao mara nyingi hucheza total football ni wazuri sana kwenye kumiliki mpira wakifanya pressing na cut off.
Idara ya kiungo ya Simba hii ndio hufanya kazi kubwa ya kuzuia na kuchezesha timu, Jonas Mkude amekuwa ndio nguzo ya Simba katikati ya kiwanja,  huyu ni defensive midfielder aliyakamilika vizuri kabisa kwasasa nchini akichangamana na watu kama Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto na Shiza Kichuya. Nyota hawa huunda muunganiko mzuri sana wa kimbinu kutokea kwenye eneo la kiungo, Shiza Kichuya ambaye mara nyingi hucheza kama invisible attacking midfield ni wazi atakuwa chachu ya mashambulizi ya Simba kutokea pemben.
Idara ya ushambuliaji ya Simba wanaonekana kucheza kwa utulivu mkubwa kutokana na uimara wa kimbinu kutoka kwa viungo wao, muunganiko huu huwafanya Ibrahim Ajib na Laudit mavugo kuwa hatari. Ni wazi walinzi wa Mbeya City watatakiwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa viungo wao wa kati ili kukata muunganiko huu wa kimbinu.
Idara ya ulinzi ya Simba ambayo ina walinzi wengi hawana kasi nzuri kwenye marking na sio wazuri sana kwa kucheza high balls,  hii inaweza kuwa faida nzuri kwa mbeya city hasa kama Mwalim wao, Mmalawi, Kinnah Phiri,  ataingia na Plan B ya kujaza viungo washambuliaji wenye kasi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video