KIKOSI cha Mbeya City FC, 'Wana komakumwanya' kesho kinatarajia kushuka katika uwanja wa Sokoine,Mbeya, kucheza mchezo mwingine muhimu wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya wageni Stand United kutoka mkoani Shinyanga
kikiwa bila nyota wake kadhaa wa safu ya ulinzi.
Kwa mujibu wa Ofisa habari, Dismas Ten, maandalizi kuelekea
mchezo huo yamekamiliki na City itashuka dimbani ikiendelea kuwakosa
nyota wake wawili wa safu ya ulinzi, Haruna Shamte na Sankhani
Mkandawile ambao waliumia kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Ruvu
uliochezwa Mlandizi mkoani Pwani na City kufungwa mabao 2-0.
“Kwenye kikosi tunaendelea kuwakosa Haruna na Sankhani,
hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha lakini taarifa njema ni
kuwa mlinzi Rajab Zahir amerejea kikosini kuongeza nguvu baada ya
kushindwa kumaliza dakika 90 za chezo dhidi ya Mwadui kufutia maumivu ya
kifungo cha mguu, madaktari wamethibitisha kuwa yuko safi na tayari kwa
mchezo wa kesho”, alisema.
0 comments:
Post a Comment