Friday, October 14, 2016

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema yeye ndiyo mchezaji bora duniani kwa sasa na kuongeza kuwa juhudi zake za kupambana kila siku ndizo zinamfanya awe alipo.

Mreno huyo kwa sasa ndiyo anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or baada ya kushinda mataji ya Champions League na Euro 2016.

"Akilini mwangu nawaza mimi ndiyo mchezaji bora wa dunia," amesema na kuongeza: "Nafanya juhudi kubwa sana kila siku ili nizidi kuwa imara. Sasa kilichobaki ni juu ya wengine kunijaji.

"Siku zote nimekuwa ni mtu ninayetaka kuimarika. Nafarijika na naamini kwamba hiyo ndiyo sababu kubwa ya mafanikio yangu uwanjani."

Mwanzoni mwa msimu huu, Ronaldo amepata wakati mgumu kutokana na kukaa nje kuuguza majeraha yake ya goti aliyopata wakati wa Michuano ya Euro mwaka huu nchini Ufaransa, lakini ameanza kurudi kwenye ubora wake baada ya kufanya vyema akiwa na timu yake ya taifa.

"Niliumia sana kwenye Michuano ya Euro mwaka 2016 na kukaa nje kwa muda wa miezi miwili na nusu, lakini kwa sasa najisikia vyema."

"Nimerejea katika ubora wangu wa kawaida na niko tayari kufurahia msimu mzuri mwingine."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video