Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameiondoa Chelsea katika mbio za ubingwa wa Premier League msimu wa 2016-17.
Akifanya mahojiano maalum na Kicker, Ferguson alitetea mwenendo wa Man United licha ya kuwa alama sita nyuma ya vinara wa ligi hiyo.
Mscoltand huyo anaamini kwamba timu zinazowania ubingwa msimu huu ni pamoja na Manchester City ambao ndio wenye nafasi kubwa, Liverpool, Arsenal na Tottenham.
Lakini ameonekana kuiondoa Chelsea, licha ya vijana hao wa Antonio Conte kushika nafasi ya nne, nyuma ya vinara Manchester City, wakiwa wametoka kuwafunga Man United 4-0 wikiendi iliyopita.
"Ni vigumu sana kutabiri kuliko ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita," alisema.
"Nadhani kuna timu kama tano hivi zinazopigania taji: Manchester City ambao wana nafasi kubwa zaidi, Tottenham na Liverpool lakini pia Man United bado wana nafasi kama watakuwa na mfululizo wa matokeo mazuri.
"Hata kama uko nyuma kwa alama sita au nane, bado kuna uwezekano wa kuwafikia wapinzani wako. Uhasama na upinzani uliopo kati ya Guardiola na Mourinho unaongeza utamu wa mashindano, lakini pia usisahau kuhusu Arsenal."
0 comments:
Post a Comment