Monday, October 17, 2016

Na Abdallah Salehe-Mdau wa MPENJA SPORTS

Ni wazi  unapolizungumzia Soka la Uingereza hutoacha kuzitaja timu hizi zenye uhasimu mkubwa wa kuwania mataji katika soka la England, Liverpool na Manchester United.
Majogoo wa Jiji ambao wapo nyumbani kwao Anfield wanaoonekana kuwa kwenye kiwango bora dhidi ya mashetani wekundu ambao bado hawajawa sawa kiuchezaji kama timu.
Huu ni mchezo utakaokuwa na ushindani mkubwa wa kimbinu na kiufundi kwa kuangalia ubora wa vikosi na falsafa za makocha wa timu zote mbili.
Juggen klopp anaependelea zaidi kutumia mfumo wa 4-3-3 huku akiwa hana mchezaji mgumu ili kuruhusu pressing game kwa kiasi kikubwa katika eneo la mpinzani na kumzuia asiingie kwenye eneo lao katika mfumo huu anaibuka na falsafa ya geggenpressing.
Ubora wa Liverpool ni wazi unaanzia kwenye safu yake ya kiungo,  watu kama Jordan Henderson na Wijnaldum, wamekuwa na muunganiko mzuri sana wa kimbinu. Wijnaldum na Adam Lallana ni wachezaji wa mbele lakini klopp huwatumia katikati pembeni ili kuifanya liverpool kuwa na wachezaji wengi wanaozunguka uwanja kwa umbali mrefu,  hivyo kuwa na eneo kubwa la kushambulia.
Idara ya ushambuliaji ya Liverpool inaonekana kuwa katika ubora mzuri,ikicheza kwa utulivu mkubwa,  watu kama Sadio Mane,Fellipe Coutinho na Roberto Firmino wamekuwa na impact kubwa kwenye kikosi huku wakipata backup kubwa kutoka kwa viungo wa nyuma.
Idara ya ulinzi ya Liverpool hii inaonekana haipo vizuri, makosa binafsi, kushindwa kujipanga kwa wakati hasa katika mashambulizi ya kushtukiza ni mambo ambayo yamekuwa yakiisumbua sana safu ya ulinzi ya Liverpool.
Ni wazi katika mchezo wa huo watatakiwa  kuwa makini sana wakizingatia wanakutana na United ya Mourinho,  mtu ambae anajua sana soka la mbinu, hivyo klopp atatakiwa kuipanga vyema safu hii huku akihakikisha Henderson aachi nafasi kubwa kati yake na idara ya ulinzi.
Kwa upande wa Jose Mourinho huyu anasifika sana kwa soka la mbinu huku akionekana kuwa muumini mzuri wa defensive game,  ni mwepesi wa kusoma mbinu za mpinzani na kuziharibu, hupendelea zaidi kutumia mfumo wa 4-2-3-1,  hapa anaibuka na falsafa ya soka la kujihami kimbinu.
Manchester United ambayo inaonekana bado haijakaa sawa kiuchezaji kama timu inaonekana inakosa muunganiko mzuri wa kimbinu hasa kutokea kwenye idara yake ya kiungo hii huifanya hata safu yao ya ushambuliaji kukosa makali ya maana.
Idara ya kiungo ya United bado inaonekana haijaimarika sawasawa kuweza kuipa nafasi kubwa ya kutawala katikati ya kiwanja,  ni wazi Mourinho atatakiwa kuzichanga vyema karata zake kwenye idara hii ili kuweza kuwabana Liverpool kwenye eneo hili. Nawaona watu kama Herrera, Michael Carrick au Morgan Shenederling , wawili kati yao wanaweza kusimama kama two holding midfielders(double pivot)
Idara ya ushambuliaji ya United kidogo inakosa muunganiko mzuri wa kimbinu hasa kutoka kwa viungo wa nyuma. Mabadiliko ya uchezaji kwa kumpanga Pogba kama attacking midfield inaweza kuwa na faida kubwa katika mchezo huo hasa kama Mourinho akiamua kutumia kutengeneza high balls plans.
Idara ya ulinzi ya  Manchester United nayo inaonekana kuwa na matatizo ya uchezaji, makosa binafsi yamekuwa yakigharimu sana timu hiyo, Erick Bailly anaonekana kuwa na kasi nzuri sana kwenye marking na amekuwa akifanya kazi kubwa lakini  kukosa msaada wa maana na ni wazi viungo wa kati watatakiwa kutoa msaada mkubwa kwa safu yao ya ulinzi ili kuua muunganiko wa kimbinu wa washambuliaji wa Liverpool.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video