Saturday, October 1, 2016

Na Rashid Salehe-Mdau wa MPENJA SPORTS

Binafsi nafikiri mchezo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuangalia ubora wa kila kikosi hasa ikizingatiwa timu hizi zimekuwa zikitumia mfumo unaofanana huku zikitofautiana kwenye pattens za uchezaji na kubadilika kutokana na hali ya mchezo.
Kwa upande wa Simba ambao wanaonekana kuwa na mabadiliko makubwa ya uchezaji, wakimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga,ubora wa Simba upo kwenye idara yake ya kiungo inayoongozwa na Jonas mkude, huyu ni defensive midfield aliyekamilika vizuri akifanya blocking na kupokonya mipira huku akiisukuma timu juu.
Hili ni eneo ambalo Simba wanaweza kuwa na faida kubwa kama wakitulia kutokana na Yanga kukosa kiungo wa aina hii ili kumzuia asitawale.
Ni wazi Omog atatakiwa kuipanga vyema safu hii kwa kumuanzisha Mkude kucheza pamoja na Mzamiru Yassin, Mnyate na Shiza Kichuya kwenye flanks huku Ajib akicheza false 10 ili kupata muunganiko mzuri wa kimbinu na kuipa uhai mkubwa safu ushambuliaji.
kwenye safu ya ulinzi, Simba wanatakiwa kuwa makini sana na aina yao ya ukabaji, mara nyingi huonekana kukabia chini na walinzi wake wengi wanaonekana kukosa kasi nzuri kwenye marking.
Kwa upande wa Yanga ambao mara nyingi hucheza direct kwa kuhama box to box huku wakijenga mashambulizi ya kasi kutokea pembeni, bado safu ya ushambuliaji inaonekana kuwa na uhai mzuri hasa wakipata msaada mkubwa kutoka kwa viungo wa kati, Kamusoko na Niyonzima bila kusahau pembeni Msuva na Kaseke wanaweza kuisumbua sana safu ya ulinzi ya Simba.
Idara ya kiungo ya Yanga itatakiwa kucheza kwa umakini mkubwa kutokana aina ya uchezaji ya viungo wa Simba,watatakiwa kutoa msaada mkubwa kwa walinzi na kuua muunganiko wa kimbinu wa viungo wa Simba
Nafikiri Simba wakicheza kwa kutulia wana nafasi kubwa ya kupata matokeo bora!

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video