Beki wa kati wa Arsenal Laurent Koscielny amesisitiza kuwa, Olivier Giroud anaweza kurejea kikosini na kufanya vizuri baada ya kupona majeraha yake na kufanya vizuri licha ya ushindani mkubwa uliopo kutokana na uwezo mkubwa unaooneshwa na Alex Sanchez, ambaye amemfananisha na mtu anayetembea kwenye maji.
Koscielny na Giroud wamezoea wote kwa pamoja kukutana pia Timu ya Taifa ya Ufaransa lakini safari hii Giroud hatakuwepo kutokana na kuendelea kuuguza jeraha lake linalomsumbua.
Alexis amekuwa akichezeshwa kama mshambuliaji wa kati wakati huu ambao Giroud hayupo na ameonesha uwezo mkubwa sana baada ya kufunga magoli matano na kupiga pasi tano za magoli ndani ya mechi nane, lakini Koscielny anasema Giroud badoa ana nafasi ya kurejea kwenye nafasi yake.
"Tulichelewa kurejea klabu baada ya mapumziko ya Euro 2016, hivyo tulipaswa kufanya mazoezi zaidi kuweka mwili tayari," Koscielny alisema wakati alipoulizwa juu ya utimamu wa mwili wa Giroud.
"Kuna ushindani mkubwa sana kwa sasa pale mbele na ukimwangalia vizuri Alexis Sanchez ni kama mtu anayetembea juu ya maji, hivyo ni vigumu sana kumuondoa katika kikosi cha wachezaji 11 wa kikosi cha awali.
"Namjua Olivier na amekuwa akipitia nyakati ngumu sana katika maisha yake ya soka. Tunafahamu namna alivyokuwa makini kupambana na changamoto hizo na naamini atafanya vizuri kwani msimu bado mrefu.
"Atapata tu fursa ya kurejea kikosini na kujibu maswali ya watu wote uwanjani."
0 comments:
Post a Comment