Saturday, October 29, 2016

KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Zeben Hernandez, amesema kuwa mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili ndio yaliyopelekea kikosi chake kuibuka na ushindi jana dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Mabadiliko hayo aliyofanya Hernandez ni ya kuwaingiza kiungo Frank Domayo, mshambuliaji Shaaban Idd na Khamis Mcha, huku akiwatoa Jean Mugiraneza, mshambuliaji Gonazo Ya Thomas na beki Gadiel Michael, ambapo yaliongeza kasi ya mashambulizi kuelekea langoni mwa Kagera Sugar.

Azam FC iliweza kufunga mabao mawili ndani ya dakika 10 za mwisho za mchezo huo, ikianaza kusawazisha kwa kufunga bao la pili lililofungwa na Domayo dakika ya 80 kabla ya nahodha John Bocco ‘Adebayor’ kufunga la ushindi dakika ya 86 baada ya kuunganisha kwa kichwa safi mpira wa krosi uliopigwa na Shaaban Idd.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Hernandez, alisema kuwa wachezaji wake walijitahidi kupambana kwenye mchezo huo kwa kila mmoja akionyesha jitihada zake binafsi na hatimaye kuvuna pointi tatu ambazo zinazidi kukikongezea morali kikosi chake.

“Kiukweli ni kwamba tunashukuru kwa sababu tumepata pointi tatu, kitu ambacho kinatufanya kuwa na morali kubwa kuweza kuendelea na mechi zijazo za ligi, wachezaji wamejaribu kusahau yale yaliyopita pia ukizingatia kikosi kina majeruhi ambao ni wachezaji muhimu kama Kapombe (Shomari) na Kangwa (Bruce), lakini wameweza kujituma na kupata pointi tatu jambvo ambalo limetufanya kusogea juu kwenye msimamo wa ligi,” alisema.

Alisema timu kwa ujumla ilifanikiwa kucheza vizuri huku akibainisha kubwa uhai zaidi uliongezeka kwa kikosi chake baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa nyakati tofauti kipindi cha pili.

“Kwa ujumla timu ilicheza vizuri kwa kila mchezaji kuonyesha jitihada zake, kitu ambacho nashukuru zaidi ni mabadiliko tuliyofanya kipindi cha pili ndizo zilienda kuongeza uhai wa timu na kuondoka na pointi tatu, alipoingia Domayo, alipoingia Shaaban, alipoimgia Mcha, naaamini ya kwamba kwa ushindi huu tulioupata tunakwenda kupumzika ikiwemo kujiandaa na mchezo unaokuja mbele,” alisema.

Ushindi huo umeifanya Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi kinachoburudisha koo cha Azam Cola na Benki bora kwa sasa nchini ya NMB yenye usalama kwa fedha zako, kufikisha jumla ya pointi 19 ikipanda hadi nafasi nne baada ya kuzishusha Mtibwa Sugar (17) na Kagera Sugar (18).

Azam FC yaanza safari kuzifuata Mbao, Toto

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC leo saa 1 asubuhi kimeanza safari ya kuelekea mkoani Mwanza, kucheza mechi mbili za ligi dhidi ya wenyeji wao Toto African (Novemba 2, mwaka huu) na kumaliza kazi ya kuwania pointi tatu muhimu jijini humo kwa kuvaana na Mbao FC (Novemba 6) kabla ya wenda mkoani Shinyanga kukipiga na Mwadui ya huko Novemba 9 ndani ya Uwanja wa Mwadui.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video