Mshambulizi nyota waYanga Amissi Jocelyn Tambwe amesema kwamba mbio za ufungaji bora ni ngumu kutokana na ushindani uliopo lakini ameahdi kupambana na kuhakikisha anatetea kiatu chake,
Tambwe, ambaye kwenye mchezo wa leo kati ya Yanga na JKT Ruvu amefunga mabao 2 kati ya 4 baada ya kuingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mzimbabwe Donald Ngoma, amesisitiza kuwa kujituma kwa bidii na ushirikiano kutoka kwa wenzake ndio vinachangia shabaha yake langoi mwa wapinzani.
"Kwanza nashukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kufunga mabao mawili kwani haikuwa kazi rahisi ukizingatia kwamba nimetoka kuwa majeruhi halafu magoli yenyewe nimefunga kipindi cha pili.
"Yote haya yanakuja kutokana na bidii yangu, kujituma na kushirikiana vyema na wenzangu ndio kumeniweka hapa.
Ameongeza kuwa safari hii ushindani umezidi kuwa mkubwa mno kutokana na wachezaji wengi kujitahidi kufunga mabao mengi ukilinganisha na msimu uliopita.
"Kwa sasa nimefikisha magoli sita na naamini mbio za kutetea kiatu changu bado ndefu kutokana na ugumu wa ligi ila naamini mpaka mwisho nitafanikiwa kutetea kiatu changu."
Kwa sasa Tambwe anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji nyuma ya nyota wa Simba aliye kwenye kiwango bora kwa sasa Shiza Kichuya mwenye magoli 7.
0 comments:
Post a Comment