Legend wa Newcastle United Alan Shearer amekuja na habari mpya iliwastua wengi kwa kusema kuwa kwenye Ligi Kuu ya England kuna mchezaji mmoja tu mwenye uwezo wa kucheza timu yoyote ulimwenguni ambaye ni Sergio Aguero.
Licha ya vilabu vingi kumwaga pesa kwa ajili ya usajili wa wachezaji mbalimbali, mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa England amesisitiza kuwa straika huyo wa Kiargentina ndiyo mchezaji pekee ambaye anaweza kuamua ubingwa kwenye timu.
Aguero alifunga mara mbili kwenye mchezo ambao Manchester City ilishinda mabao 4-0 dhidi ya West Brom kwenye Uwanja wa Hawthorns, hali iliyompelekea Shearer kusema maneno hayo.
Akiongea kwenye Match of the Day, Shearer amesema: "Ni moja ya wachezaji waliojipambanua kuwa bora na wa kiwango cha dunia, nadhani ndio hyuo pekee tuliye naye hapa Premier League na ni mshambuaji bora kabisa wa kati kwa sasa kwenye ligi."
Alipoulizwa na Gary Lineker sababu gani zinamfanya aseme hivyo, Shearer aliendelea kumtetea kwa kusema: "Unapoangalia rekodi zake na baadhi ya magoli anayofunga na aliyofunga huwezi kukaa ninachosema.
"Kwa kifupi ni mchezaji wa kiwango cha dunia."
It's a big shout from Alan Shearer.... https://t.co/tHyabgHtso— Match of the Day (@BBCMOTD) October 29, 2016
0 comments:
Post a Comment