Tuesday, October 11, 2016

Nahodha wa England Wayne Rooney amesisitiza kuwa hana mpango wowote wa kustaafu soka la kimataifa kufuatia kuondolewa kikosi kwenye Timu ya Taifa ya England.

Rooney, 30, hataanza kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Slovenia utakaochezwa leo baada ya meneja Gareth Southgate kumwacha mchezaji huyo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo.

Licha ya kujikuta kuwa na wakati mgumu kwenye klabu na taifa lake, Rooney anaamini kwamba bado ana mchango mkubwa huku akimtaja Ryan Giggs kama mfano wake.

"Unajua haya ni mambo ambayo kama binadamu napaswa kupitia," alisema Rooney ambaye mpaka sasa amefunga goli moja kwenye 12 aliyoichezea United msimu huu.

"Naamini naweza kurudi kwenye kiwango changu. Nina umri wa miaka 30 kwa sasa. Sina miaka 35 au 36 ambayo pengine ningesema kwamba nimekwisha. Nitaendelea kujituma kwa bidii kama nilivyosema awali kwamba sitaacha kulitumikia taifa langu."

Wakati Ryan Giggs ana miaka 30 hakuwa yuleyule pindi alipokuwa na miaka 18 na aliweza kucheza mpaka alipokuwa na miaka 40. Kuna mifano mingine mingi tu. Naamini itakuwa hivyo kwangu pia. Mimi sio mjinga linapokuja suala la kufikiria. Nafahamu vizuri kwamba niko tofauti na nilipokuwa na miaka 20, lakini bado naamini nina ubora wa kuweza kuisaidia timu hii katika siku zijazo."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video