Monday, October 3, 2016

Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' jana walipoteza nafasi ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana Chini ya miaka 17 baada ya kufungwa bao 1-0 na Congo Brazzaville


Serengeti Boys wamejikuta wakitupwa nje kwa faida ya goli la ugenini kufuatia mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa kushinda kwa mabao 3-2, hivyo Congo kuwa na wastani mzuri wa magoli ya ugenini.


Baada ya hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi ameonesha kusikitishwa na matokeao hayo huku akielezea nambna vijana pia walivyoumizwa mpaka kufikia hatua ya kulia punde tu baada ya mchezo kumalizika.

Malinzi amesema: "Poleni kwa matokeo ya jana. Baada ya mechi vijana walilia sana. Imeumiza lakini ndio mpira.Timu itatua kesho jumanne usiku sa3 kwa Rwanda air. Jumatano tutakula nao chakula cha mchana na kuwaeleza nini matarajio yetu kwao. Na kikubwa watajulishwa kwamba wao sasa ndio Ngorongoro Heroes ya 2019. Taratibu tutajenga Taifa stars ya 2021 kwa kuwashirikisha kwa karibu vijana hawa. Kikubwa ni sisi viongozi kutokaa nao mbali na kuzidi kuwapatia mechi hasa za kimataifa. Ni muhimu wakue pamoja."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video