Kichuya Jana amefunga goli lake la kwanza kwenye mchezo wa watani wa jadi
tangu asajiliwe Simba kwenye dirisha la usajili lililopita, huu ni msimu
wake wa kwanza akivalia jezi nyekundu katika michezo ya ligi kuu
Tanzania bara.
Tovuti ya shaffihdauda.co.tz aliripoti kuwa baada ya kupiga kona iliyozama moja kwa moja wavuni, alisema mechi
ilikuwa ngumu lakini anashukuru timu yake angalau imepata pointi moja.
“Nashukuru Mungu kwasababu tulikuwa tunatafuta pointi, mimi nimefunga
goli ili kuisaidia timu yangu lakini si kupata sifa, lengo lilikuwa
kupata pointi tatu lakini Mungu katujaalia tumepata pointi moja
tunashukuru”, alisema mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ya
Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Kichuya amesema mechi ilikuwa ngumu lakini kitu anachoshiru ni kumalizika salama kwa mchezo huo uliokuwa na presha kubwa.
“Mechi ilikuwa ngumu lakini nashukuru mchezo umemalizika salama.”
Mechi za Simba na Yanga huwa zinapresha yake, kwa upande wa Kichuya
yeye amese hivi: “Mechi ilikuwa ni ya kawaida tu kama mechi nyingine.”
Nikamwambia atoe neno kwa mashabiki wake na Simba kwa ujumla baada ya
kumalizika kwa mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi
wa soka la Bongo.
“Wakae wasubiri mambo mengi yanakuja kutoka kwenye timu yao ya sasahivi.”
0 comments:
Post a Comment