Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba ambaye ni pia ni Mwanachama wa Yanga, amesaidia kumrejesha kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyo mapema wiki hii.
Katika mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.
Wakati huo huo, Yanga nayo imemuandikia barua ya kumjibu kocha wake, Pluijm juu ya ombi la kujiuzulu ikitaa ombi hilo.
Katika barua iliyosainiwa na Katibu, Baraka Deusdedit, Yanga imesema haioni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo baada ya mafanikio aliyoipa klabu.
Mholanzi huyo alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu, akisema huko ni kumvunjia heshima.
Kocha huyo akakataa hadi nafasi ya Ukurugenzi wa Ufundi amabyo inasemekana Yanga ilitaka kumpa baada ya kumleta Lwandamina kuwa kocha Mkuu.
Pluijm amezungumza na MPENJA SPORTS mchana huU akisema amekubali kurejea kazini kwake kama kawaida.
"Ni kweli nimerejea katika nafasi yangu baada ya mazungumzo na watu marafiki wa Yanga (Mwigulu Nchemba) ambao wameniomba sana nirejee Yanga, nimekubali. kesho nitaanza kazi na Jumapili nitakuwepo kwenye mechi ya Ligi kuu dhidi ya Mbao'. Amesema Hans van der Pluijm akizungumza na MPENJA SPORTS.
0 comments:
Post a Comment