Friday, October 14, 2016



MECHI ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons iliyotakiwa kuchezwa kesho (Jumamosi) Uwanja wa Manungu, Morogoro, imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itachezwa siku ya Jumapili.
Sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo haijawekwa wazi na Bodi ya Ligi ambayo mara kwa mara imekuwa ikipangua ratiba ya VPL.
Hata hivyo, mechi nyingine za VPL zitaendelea kesho (Jumamosi) kama kawaida,  Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, JKT Ruvu wataikabili Mwadui FC, wakati huko Kambarage Shinyanga, Chama la Wana, Stand United watakuwa wenyeji wa African Lyon.
Toto African watakuwa Uwanjani kwao CCM Kirumba kuchuana na Wanalizombe, Majimaji FC.
 
JUMAPILI, michezo mingine itakuwa kati ya Azam FC na Yanga Uwanja wa Uhuru, huku Maafande wa Ruvu Shooting wakipepetana na Ruvu Mbeya City.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video