Nahodha wa Mbeya City Fc , Kenny Ally ameipogeza timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa hatua nzuri waliyofikia licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Afrika kufuatia kufungwa bao la dakika za lala salama walipokuwa kwenye mchezo wao wa mwisho huko Jamhuri ya Congo.
“Kifupi nawapongeza, wamefanya kazi kubwa sana, hatua
waliyofikia ni ya kujivunia kwa sababu wametengeneza mwanga mzuri kwenye
mashindano mengine yatakayokuja, hii ni tafsiri kuwa Shirikisho letu
lilikuwa na nia ya dhati ya kuhakikisha tunafanikiwa, kilichotokea ni
sehemu ya mchezo wa soka” alisema.
Kenny Ally ambaye alikuwa ni mmoja wa nyota wa timu ya Taifa ya
Tanzania waliokwenda nchini Brazil na kutwaa kombe la Copa Coca cola
licha ya kutoa pongezi wa Shirikisho pia alitoa wito kwa Rais Jamal
Malinzi kuhakikisha anaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu nzuri ya
taifa siku za usoni.
“Nampongeza Rais (Malinzi) na ninatoa wito tu kuhakikisha
wanaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu bora ya Taifa siku zijazo,
nakumbuka hali iliyotokea kwetu sisi tulioenda Brazil na timu ya vijana,
baada ya kurudi na kombe hakuna jambo lolote lililoendelea na matokeo
yake timu ile ikafaa na wachezaji tuliokuwepo kusambaa hovyo na hivi
sasa kuna ambao wameshaacha soka na wachache tumebaki tunaendelea
kucheza”‘ alimaliza.
0 comments:
Post a Comment