Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Simba SC, MUSLEH AL RAWAHI.
Uongozi wa klabu ya Simba umeunda Kamati mpya ya Mashindano, ambayo itakuwa chini ya Mwenyekiti, Musleh Al Rawahi.
Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Haji Sunday Manara, amekaririwa na Blog ya Michezo ya Salehjembe akisema kuwa Kamati hiyo imeundwa
ili kuongeza nguvu katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu.
Manara
amesema pamoja na Musleh ambaye ni Mwenyekiti amewataja wajumbe wengine
katika Kamati hiyo kuwa ni Makamu Mwenyekiti, Hassan Hassanoo na
Wajumbe; Mohamed Nassor “kigoma”, Dk Cosmas Kapinga, Juma Abbas Pinto na
Octavian Mushi.
Musleh
ni kati ya wanachama wakongwe kabisa wa Simba na amekuwa anakumbukwa na
wengi kutokana na ule uamuzi wake wa kumpa gari aliyekuwa kiungo wa
Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ kutokana na juhudi na maarifa alizokuwa
akionyesha wakati huo.
Kamati hiyo, imeelezwa itakuwa ikifanya kazi ya kuratibu masuala mbalimbali yanayohusiana na mashindano.
Musleh pia amewahi kuwa kwenye kamati ya usajili ya Simba na kamati nyingine mbalimbali.
Pia Hassanoo ambaye maarufu kama kama Mpiganaji, pia amewahi kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment