HUU HAPA MTIFUANO WA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Alhamisi Oktoba 6
KUNDI D
Austria v Wales
Moldova v Serbia
Republic of Ireland v Georgia
KUNDI G
2145 Italy v Spain
Liechtenstein v Albania
Macedonia v Israel
KUNDI I
Iceland v Finland
Kosovo v Croatia
Turkey v Ukraine
..............................................
BAADA ya kuchezwa Mechi za Kwanza za Makundi ya Nchi za Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia Mwaka 2018, Mataifa ya Ulaya Leo yanaanza raundi nyingine ya Mechi zao za Pili za Makundi ambazo Wiki ijayo zitapigwa zile za Tatu.
Mechi kubwa kabisa kwenye michuano hii hivi sasa ni ile ya Leo huko Juventus Stadium Jijini Turin Nchini Italy ya Kundi G kati ya Italy na Spain.
Mwezi Julai huko France, Nchi hizo zilipambana kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016 na Italy kuichapa Spain 2-0.
Hii Leo Kocha Mpya wa Italy Giampiero Venturo atamkosa nguzo yake kubwa Beki wake Giorgio Chiellini ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi G waliposhinda Ugenini 3-1 dhidi ya Israel.
Lakini Leo Italy wako kwao, Juventus Stadium, Uwanja ambao una Mashabiki waliokubuhu na ni dimba ambalo hawajafungwa hata Mechi moja.
Spain, chini ya Kocha Mpya Julen Lopetegui, walianza Kundi G kwa kishindo wakiwa kwao kwa kuichabanga Liechtenstein 8-0 na hii Leo Kocha huyo amethibitisha kuwa Straika wa Chelsea Diego Costa ataanza Mechi hii.
.........................
JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 wa Makundi watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia
....................
Kesho Ijumaa, kwenye Kundi A, France ambao walianza kwa Sare ya 0-0 na Belarus Leo wako kwao kucheza na Bulgaria walioanza kwa ushindi wa 4-3 dhidi ya Luxembourg.
England, ambao wako Kundi F na walianza kwa kuifunga Ugenini 1-0 Slovakia, wapo kwao kucheza na Malta iliyoanza kwa kuchapwa Nyumbani kwao 5-1 na Scotland.
Scotland watacheza Jumamosi wakiwa kwao dhidi ya Lithuania ambayo ilitoka Sare 2-2 na Slovenia ambao nao Siku hiyo hiyo wako kwao kuivaa Slovakia.
Mechi hizi za Kanda ya Ulaya kwa Kipindi hiki zitakamilika Jumanne Oktoba 11.
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Ijumaa Oktoba 7
KUNDI A
France v Bulgaria
Luxembourg v Sweden
Netherlands v Belarus
KUNDI B
Hungary v Switzerland
Latvia v Faroe Islands
Portugal v Andorra
KUNDI H
Belgium v Bosnia-Herzegovina
Estonia v Gibraltar
Greece v Cyprus
Jumamosi Oktoba 8
KUNDI C
1900 Azerbaijan v Norway
Germany v Czech Republic
Northern Ireland v San Marino
KUNDI E
1900 Armenia v Romania
1900 Montenegro v Kazakhstan
Poland v Denmark
KUNDI F
1900 England v Malta
Scotland v Lithuania
Slovenia v Slovakia
Jumapili Oktoba 9
KUNDI D
1900 Wales v Georgia
Moldova v Republic of Ireland
Serbia v Austria
KUNDI G
1900 Israel v Liechtenstein
Albania v Spain
Macedonia v Italy
KUNDI I
1900 Finland v Croatia
1900 Ukraine v Kosovo
Iceland v Turkey
Jumatatu Oktoba 10
KUNDI A
Belarus v Luxembourg
Netherlands v France
Sweden v Bulgaria
KUNDI B
Andorra v Switzerland
Faroe Islands v Portugal
Latvia v Hungary
KUNDI H
Bosnia-Herzegovina v Cyprus
Estonia v Greece
Gibraltar v Belgium
Jumanne Oktoba 11
KUNDI C
Czech Republic v Azerbaijan
Germany v Northern Ireland
Norway v San Marino
KUNDI E
1900 Kazakhstan v Romania
Denmark v Montenegro
Poland v Armenia
KUNDI F
Lithuania v Malta
Slovakia v Scotland
Slovenia v England
0 comments:
Post a Comment