Monday, October 24, 2016

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameachana na klabu yake ya TP Mazembe ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya mkataba wake kumalizika.
Taarifa iliyopenyezwa kwa MPENJA SPORTS na moja ya watu wanaomsimamia Ulimwengu imesema kuwa wamefikia maamuzi ya nyota huyo kutosaini tena Mazembe kwasababu ya kuepuka usumbufu kama walioupata kwenye harakati za kumuuza Barani Ulaya, Mbwana Samatta .
Kiongozi huyo amesema walikuwa wamepata timu nyingi zilizokuwa zinamhitaji Samatta, lakini Mazembe walimbania kwa vile walikuwa na mkataba naye na walimuachia wakati mkataba wake unaelekea kumalizika kwani walijua fika mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji asingesaini mkataba mpya na angeondoka akiwa huru.
Vivyo hivyo kwa Ulimwengu tayari kuna timu zinamhitaji kwasasa (Hazijatajwa) na ili kufikia malengo yake, ni bora aachane kabisa na Mazembe.
Ulimwengu tayari amewasili Jijini Dar es salaam akisubiri mambo yake yakae sawa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video