Taarifa zilizoifikia Mpenja Sports hivi punde zinadai kuwa Kocha mkuu wa Yanga, Hans Van der Pluijm amefikia uamuzi wa kujiuzulu kufuatia kuwasili kwa kocha mpya Mzambia George Lwandamina ambaye inaelezwa atachukua nafas yake.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa Lwandamina tayari amesaini makataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo na iliamuriwa kwamba Pluijm angepewa nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa benchi la ufundi.

Kwa mujibu wa Pluijm, ameona ni vyema ajiuzulu kwa kwa kuwa asingependa kubaki kama Mkurugenzi wa Ufundi ilhali bado ana nguvu za kuweza kutimiza majukumu yake uwanjani.
Pluijm anasema kwa sasa amebakiwa na mechi tatu tu mkononi ambapo akimaliza michezo hiyo, basi ataachana na timu hiyo.
"Sijaona wala kuthibitisha kwa MTU ila nimeamua kujiuzulu, nimesoma mengi baada ya mechi ya Jumamosi..lakini leo asubuhi nimeenda Ofisini kupeleka barua yangu, mlango mmoja unapofungwa Mwingine hufunguliwa, naifahamu Kazi yangu". Hans van der Pluijm akiongea na Mpenja Sports.
0 comments:
Post a Comment