Manchester United wanaikaribisha Manchester City leo katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la Ligi maarufu kama EFL, mchezo utakaofanyika kunako Uwanja wa Old Trafford saa 4 kamili usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.
Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne hatakuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na jeraha la mguu.
Pablo Zabaleta pia atakosekana lakini Vincent Kompany, ambaye wikiendi iliyopita kwa mara ya kwanza alicheza mchezo wa ligi tangu April yuko fiti kuwakabili mahasimu wao.
City hawashinda takriban michezo mitano kwenye michuano yote na meneja wao Pep Guardiola ataendelea kufanya rotation ya kikosi chake.
"Baadhi watacheza leo. Nahitaji kuona wachezaji mazoezini halafu ndiyo natoa maamuzi yupi acheze na yupi asicheze," amesema."
United pia mwezi huu bado hawaonja ladha ya ushindi kwenye ligi mwezi huu ikiwa ni pamoja na kupewa kipigo cha aibu cha magoli 4-0 kutoka kwa Chelsea Jumapili, lakini Guardiola amesema "mara zote amekuwa akiwaheshimu wapinzani wake"
"Ni timu yenye ubora wa hali ya juu. Tumewazidi alama, ikiwa ni sawa uwiano wa michezo miwili tu," amesema Guardiola ambaye kwenye mchezo wa Premier League waliokutana mwezi September alishinda 2-1.
"Michezo ya mahasimu ina uzito wa kipekee. Tutajaribu kucheza kwa umakini wa hali ya juu ili kupata matokeo."
Guardiola ameongeza kwa kusema kuwa angependa kuona mshambuliaji wake raia wa Argentina Sergio Aguero, ambaye amekuhuwa akihusishwa na kuhama klabuni hapo akibaki kwa muda mrefu zaidi".
"Nina furaha sana na Sergio. Ningependa kumwona anabaki na kuendelea kucheza pamoja nasi. Ni mchezaji wa aina yake," Guardiola amesema.
Match facts
- Manchester United wameshinda mechi mbili tu Kombe la ligi kati ya sita zilizopita dhidi ya Manchester City (sare 1, kufungwa mara 3), japokuwa hawajapoteza mechi tatu walizokutana Old Trafford.
- Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana kwenye Kombe la Ligi ilikuwa ni msimu wa 2009-10 kwenye nusu fainali ambapo United walishinda kwa wastani wa magoli 2-3, baada ya kushinda 3-1 Old Trafford.
- Mara zote ambazo Man City wamewaondosha mahasimu wao mashindanoni kwenye Kombe la Ligi, wamefanikiwa kubeba kombe hilo (1969-70 na 1975-76).
- Kwenye michuano yote, Man City wameshinda mechi nne kati ya sita zilizopita katika Uwanja wa Old Trafford (sare 1, kufungwa mara 1)).
- Ushindi mara mbili kati ya tatu wa Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola kama meneja umetokana na mechi za michuano ya ligi (mara moja kwenye Champions League, na mwingine kwenye Kombe la Copa Del Rey).
- Kwenye michuano yote, Guardiola ameshindwa kupata matokeo kwenye mechi tatu za ugenini akiwa na Man City. Amewahi kucheza mechi nne za ugenini bila ushindi katika historia ya maisha yake ya ukocha (ilikuwa ni mwezi March 2009).
0 comments:
Post a Comment