Wednesday, October 12, 2016

Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amefunga goli lake la kwanza tangu alipotua kwenye klabu hiyo kabla ya msimu huu kuanza alipojumuishwa kwenye kikosi cha Jangwani kikiwa kwenye michuano ya Caf.

Chirwa alifunga goli lake la kwanza kwenye msimu huu ikiwa ni mechi ya saba kwa Yanga katika ushindi wa mabao 3-1

Mzambia huyo aliunganisha mpira uliochelewa kuokolewa na mabeki baada ya kupigwa kona iliyookolewa lakini mpra ukamkuta Simon Msuva ambaye alipiga goli kwa Mtibwa na kuzua piga nikupige.

Yanga imefanikiwa kupata ushindi tangu ilipoifunga 2-0 Mwadui FC, ilipoteza 1-0 dhidi ya Stand United, ikatoka sare ya kufungana 1-1 na Simba October Mosi.

Chirwa alifunga bao hili dakika ya 45 na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kutulia na kusawazisha bao safi kupitia kwa Haruna Chanongo baada ya kutumia vyema uzembe wa mabeki wa Yanga Kelvin Yondani na Adrew Vincent 'Dante'

Yanga walikuja juu na kuongeza bao la pili kupitia kwa Simon Msuva aliyeambaa na mpira winga ya kulia na kuingia eneo la hatari na kupiga shuti kali lililoingia moja kwa moja.

Donald Ngoma aliyeingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Chirwa aliifungia Yanga bao la tatu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Geoffrey Mwashiuya kutoka kushoto mwa uwanja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video