Cet Njovu (Wa pili kutoka kushoto) akipokea Jezi kwa Niaba ya Team Ismail kutoka kwa muwakilishi wa Kampuni ya BIN SLUM TYRES, Bwana Salim Said Al Jabry. Kulia ni Bi Fatma, Mratibu wa Kandanda Day
=========
Kampuni ya uuzaji matairi nchini ya Bin Slum Tyres
Ltd,imeendeleza utamaduni wake wa kulidhamini tamasha la ‘Kandanda Day’,ambalo
litafanyika Oktoba 15,mwaka huu katika uwanja wa Jakaya M Kikwete Park,Kidogo Chekundu.
Mratibu wa tamasha hilo,Fatma Dahir,amesema kwamba wanaishukuru
kampuni hiyo inayoongoza kwa uuzaji matairi nchini kwa msaada wa fedha na vifaa
kwa ajili ya tamasha hilo linalobebwa na kauli mbiu Dawati na Mpira.
“Kwanza kabisa tunapenda kuchukua fursa hii,kuishukuru sana
kampuni ya Bin Slum,kwa kutuamini na kuwa pamoja zaidi ya miaka miwili katika
kuhakikisha tamasha hili linaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka,”alisema na
kuongeza
“Kwa mwaka huu,kauli yetu mbiu ni Dawati na Mpira, ambayo lengo lake
kuu ni kuhakikisha sisi kama wanamichezo tunaunga mkono jitihada za Serikali
katika kuhakikisha shule zetu zina madawati ya kutosha,hivyo tunaamini kwa
ushirikiano wa wanamichezo wanaounda kundi la Kandanda kwenye ukurasa wa
facebook na wadau wengine,tunaweza kuchangia kitu kwa ajili ya elimu yetu.”
Fatma alisema,kwamba wanaamini udhamini wa fedha walioupata
kutoka Bin Slum,utakua chachu ya ulifanikisha tamasha la mwaka huu,kuwa bora
zaidi na kuweka historia kwa wanamichezo watakaoshiriki na shule itakayopata
msaada wa madawati.
Kwa upande wa mwakilishi wa kampuni ya Binslum Tyres Ltd, Bwana Salim
Said Al Jabry, alisema kwamba wameamua kuendeleza utamaduni wao wa kuchangia
tamasha la kandanda pamoja na kuuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati
nchini.
“Binslum Tyres tunafuraha kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya
udhamini,ikumbukwe huu ni mwaka wa tatu kwa kampuni yetu kudhamini
tamasha hili,ambalo kwetu ni faraja kuona wadau wanakutana pamoja na
kushiriki pia kuisaidia jamii kupitia mchezo wa kandanda,”alisema Al Jabry na
kuongeza:
“Kwa hiyo mwaka huu mbali na kutoa jezi kwa timu mbili mwenyeji
ya Team Dizo Moja na Team Ismail,lakini pia tumetoa kiasi cha fedha kipatacho
milioni moja kwa ajili ya kuchangia mchango wetu wa madawati na shughuri
zingine za uendeshaji.”
Mwaka huu tamasha hilo linatarajia kushirikisha timu mbalimbali
za makampuni ambazo zitacheza katika mfumo wa ligi,kabla ya mshindi
kupatikana katika mchezo wa fainali.
Mratibu wa Kandanda Day
Fatma Dahir
0763 600166
0 comments:
Post a Comment