Friday, October 14, 2016

 
KATIKATI ya Juma hili Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, ilikuwa muda wa neema kwa Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ambaye unaweza kusema aliondoa gundu au ukame wa mabao akifunga goli lake la kwanza Yanga iliposhinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Baada ya mafanikio hayo  Chirwa, Raia wa Zimbabwe amesema anaamini ataendelea kufanya vizuri pengine tofauti na matarajio ya wengi.

“Najua tunavyoshirikiana, tunavyofanya kazi yetu kwa pamoja kwa lengo la kuisaidia timu. Natamani kufunga, pia natamani kutoa pasi za mabao. Nitasaidiana na wenzangu na kufanya vizuri,” alisema Chirwa.

Mshambuliaji huyo alifunga bao safi la shuti kali, likiwa la kwanza kwake kwenye ligi na alikimbia kwenda kumkumbatia kocha wake, Mholanzi Hans van der Pluijm pamoja na wachezaji wengine akiwemo Donald Ngoma waliyekuwa pamoja pia kule FC Platinum ya Zimbabwe.
Pamoja na Chirwa kuonekana ni mchezaji mzuri, suala la presha limeonekana kumpa wakati mgumu na kufunga bao, huenda kukamsaidia kufanya vizuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video