AZAM FC usiku huu wakiwa Uwanjani kwao Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam wamelazimisha sare ya 2-2 na Maafande wa Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Jean Mugiraneza na Khamis Mcha, wakati ya Ruvu Shooting yamefungwa na Fully Zulu Maganga na Shaaban Kisiga.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 11 baada ya kucheza mechi saba, ikishinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Ruvu Shooting inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi saba, ikishinda mbili, kufungwa mbili na sare tatu.
Ruvu Shooting inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi saba, ikishinda mbili, kufungwa mbili na sare tatu.
Leo zimechezwa mechi 6 za Ligi kuu na yamefungwa jumla ya mabao 10.
Tazama jedwali hapo chini likionesha matokeo yote na wafungaji wa mechi zote.
0 comments:
Post a Comment