Thursday, October 6, 2016



Suala la winga wa Azam FC Farid Musa kuendelea kuwepo Bongo wakati awali ilitangazwa amefuzu majaribio kwenye klabu ya Tenerife ya Hispania limeendelea kuzua maswali ambayo imebidi mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba atoe ufafanuzi.
Tovuti ya shaffihdauda.co.tz ameripoti kuwa Kawemba amesema, Farid ni mchezaji halali wa Tenerife lakini kinachomfanya aendelee kuwaepo nchini ni suala la kibali chake cha kufanya kazi Spain kutokamilika.
“Inasikitisha kufikiria Farid anacheza Tanzania, mwenye mawazo hayo tunaomba ayafute. Sala zetu zote ni kuona Farid hachezi mpira Tanzania, inawezekana watu wengine nje ya Azam wanajaribu kumshawishi labda acheze kwenye vilabu vyao,” amesema Kawemba.
“Azam tayari tulishatoa ITC kama tungekuwa tunamtaka tusingeitoa, tumeshaitoa ipo Spain, sisi kama klabu tunapokuwa na Farid tunamwita mchezaji wa Tenerife ya Spain na sio mchezaji wa Tanzania.”
“Suala la kibali chake cha kufanya kazi ndiyo kinashughulikiwa na wenzetu wa Tenerife. Kipo nje ya uwezo wa Azam FC lakini tunatoa ushirikiano wote unaohitajika ili aende.”
“Kuna mtu anajiita wakala wake anahangaika sana kuhakikisha Farid haendi Tenerife lakini tulishamaliza hili suala.”
“Farid anakwenda Tenerif hajauzwa, anakwenda kwa mkopo kwasababu thamani yake inakua. Anakwenda kwa mkopo ili acheze wamuongezee thamani ili atakapokuwa akisajiliwa, thamani yake iwe tofauti na wakati anatoka Tanzania.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video