PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC na Ruvu Shooting linatarajia kufanyika Jumapili ijayo saa 1.00 usiku ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo, Azam FC imeweka viingilio vya kawaida kabisa vya aina mbili ili kuwapa fursa Watanzania wengi kuhudhuria mtanange huo wa kukata na shoka, ambavyo ni kama ifuatavyo:-
= VIINGILIO VYA JUKWAA KUU (V.I.P) - SH 10,000/=
= VIINGILIO VYA MZUNGUKO (OTHERS) - SH 3,000/=
Azam FC inapenda kuwafahamisha mashabiki wake na wapenzi wa soka kwa ujumla kuwa, hivi sasa mechi zake zote za nyumbani zitakazochezwa Azam Complex zinatarajia kufanyika usiku ili kuwapa fursa mashabiki wengi kushuhudia timu yao ikicheza.
Klabu hiyo bora ya Afrika Mashariki na Kati, inaamini kuwa muda huo ni muafaka kwa wapenzi wa soka kushuhudia mechi kwani wengi wao waliokuwa wakikosa fursa ya kutazama 'live' mechi za Azam FC kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi, hivi sasa watakuwa huru kuja Azam Complex kuziona mechi hizo.
0 comments:
Post a Comment