Tuesday, September 6, 2016

 Msafara wa wachezaji 20 na viongozi 7 wa Yanga umewasili salama mjini Mtwara kuelekea moja kwa moja kwenye hoteli ya Tiffany kwaajili ya mapumziko mafupi tayari kuwaa Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Nagwanda Sijaona kesho.
Mamia ya wapenzi na mashabiki wameeilaki timu hiyo kwa furaha punde tu ilipowasili hali iliyoleta faraja kwa msafara huo na kuiongezea ari ya kuibuka na ushindi hapo kesho.

Nahodha wa klabu hiyo Nadir Haroub Ali 'Cannavaro' ameguswa sana na moyo huo wa mashabiki na kuahidi kuwapa furaha hiyo kesho dhidi ya wabishi hao wa Ndanda ambao tangu wapande Yanga hajawahi kushinda kwenye uwnja huo.
"Furaha hii waliyotupokea nayo mashabiki wetu tuhakikishe inabaki kwenye nyoyo zao tutakapoondoka Alhamisi. Lazima tushinde mechi hii," alisikika Canavaro huku akiwaasa wenzake wakati wakiteremka kwenye basi.

Jioni hii Yanga wanafanya mazoezi kwenye dimba la Nangwanda Sijaona kujiweka tayri kabisa kwaajili ya mchezo wa kesho utakaofanyika majira ya saa 10:00 za jioni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video