Tuesday, September 6, 2016

Kikosi cha Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, kimeondoka leo Alfajiri kuelekea mkoani Mtwara tayari kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Ndanda utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga tangu kufunguliwa kwa pazia la ligi, wakiwa pungufu kwa mchezo mmoja na mwili kwa baadhi ya timu kutokana na kuchelewa kuanza ligi kufuatia uwakilishi wake katika michuano ya kimataifa ambapo waliishia katika hatua ya makundi.

Vilevile mchezo wao uliotakiwa kupigwa Jumatano wiki iliyopita dhidi ya JKT Ruvu uliahirishwa kutokana na kuwa na idadi ya wachezaji tisa waliojiunga na timu zao za taifa kwaajili ya michezo ya kufuzu Afcon 2018.

Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuwa mgumu wa aina yake kutokana na upinzani mkubwa unaotokea pindi timu hizo zinapokutana.

Hata hivyo kuna baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa kurudi kutoka kuyatumikia mataifa yao kwenye mechi za kimataifa na matatizo ya kifamilia.

Wachezaji hao ni pamoja na Deogratius Munishi (Msibani), Geofrey Mwashuiya (majerhi), Pato Ngonyani (majeruhi), Malimi Busungu (majeruhi), Haruna Niyonzima (timu ya taifa), Vicenti Bossou (timu ya taifa).

Wachezaji waliosafiri na timu;
Makipa: Ali Mustafa na Beno Kakolanya

Walinzi: Juma Abdul, Hassani Kessy, Haji Mwinyi,  Oscar Joshua,  Vicenti Andrew,  Kelvin Yondani, Nadir Haroub

Viungo:  Simon Msuva, Yusufu Mhilu, Mbuyu Twite, Deusi Kaseke, Juma Makapu, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi


Washambuliaji: Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Mateo Antony, Amissi Tambwe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video