Aliyekuwa meneja wa England Sam ameandika waraka wa kuomba radhi baada ya kujizulu nafasi yake kufuatia kashfa ya mbaya inayomkabili.
Allardyce ambaye amedumu kikosini hapo kwa muda wa siku 67 tu tangu abebe majukumu hayo, nafasi yake imezibwa kwa muda na meneja wa kikosi cha England chini ya miaka 21 Gareth Southgate na kumalizia michezo yote iliyosalia.
"Ilikuwa ni heshima kubwa kwangu kuteuliwa kuwa meneja wa England mwezi July na kwa hakika nimesikitishwa sana na jambo hili.
"Jioni ya leo (jana), nimekutana na Greg Clarke na Martin Glenn na kueleza azma yangu ya kuomba msamaha kwa tukio lililotokea."
"Japokuwa nimeweka wazi kwenye yale mazungumzo yaliyorekodiwa kwamba maafikiano yale yangehitaji uthibitisho ama kupitishwa na FA, lakini natambua nimetoa baadhia ya kauli ambazo zimeumiza watu," Allardyce amezidi kuelezea.
"Nikiwa kama moja ya watu waliohudhuria kikao cha leo (jana), niliambiwa nitoe ufafanuzi juu ya nilichokieleza na eneo ambalo mazungumzo hayo yalifanyika. Na nimetoa ushirikiano mkubwa sana kwenye suala hilo.
"Vilvile najutia sana kauli zangu hasa kwa kumlenga mtu mmoja-mmoja."
England watavaana na Malta kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia Oktoba 8, tayari wakiwa wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Slovakia kwa bao 1-0 wakati huo Allardyce akiwa kwenye bechi la ufundi
0 comments:
Post a Comment