Kuelekea 'Dabi' ya Manchester itakayochezwa Kesho kati ya Manchester United na Manchester City Dimbani Old Trafford, Zlatan Ibrahimovic amemsifu Jose Mourinho kuwa ni Bingwa wa kucheza na akili.
Mourinho na Guardiola wanakutana kwa mara ya kwanza katika soka la England .
Ikumbukwe Ibrahimovic hana furaha na Guardiola ambaye alimfundisha akiwa Barcelona na sasa yuko Etihad.
Msweden huyo alishindwa kutamba akiwa na Guardiola nchini Hispania baada ya mwaka 2009 kusajiliwa kwa pauni milioni 57 kutoka Inter Milan ambapo alicheza muda mfupi chini ya Mourinho.
Ibrahimovic amesema: "Mourinho ni bingwa wa kucheza na akili. Anajua kila kitu kuhusu mchezo.
'Sijutii sana, lakini najuta kwanini sikucheza muda mrefu chini ya Mourinho. Fursa ilipokuja tena ya kufanya naye kazi United, yalikuwa maamuzi rahisi sana kwangu".
'Nani ambaye hapendi kufundishwa naye? Nipo katika klabu kubwa yenye kocha mkubwa na mashabiki wakubwa , nataka kufanikiwa kadri inavyowezekana kwa ajili yao"
Guardiola ambaye anaelezwa kuwa hasama mkubwa wa Mourinho amekuwa akipokea vijembe mbalimbali kutoka watu wa upande wa Mourinho.
Wakala wa Ibrahimovic, Mino Raiola, jana alifungua mdomo wake na kuanzisha vita ya maneno dhidi ya Guardiola.
"Simpendi Guardiola". Alisema Raiola: "Simchukii, lakini simpendi. Kila mtu anajua kilichomtokea Zlatan katika klabu ya Barcelona".
"Ni kocha mzuri, lakini falsafa yake ya soka inaniboa".
0 comments:
Post a Comment