Kiungo huyo fundi amecheza baadhi ya klabu kubwa na kupata mafanikio makubwa ikiwemo Real Madrid na Bayern Munich.
Kwasasa akiwa Bayern ameungana na kocha wake wa zamani Real Madrid, Carlo Ancelotti.
Manchester derby ni leo kuanzia saa nane na nusu mchana kwa saa za Afrika Mashariki na itakuwa ya kuvutia kwasababu ya makocha wawili mahasimu kukutana , Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Man City.
Wawili hao wamehamisha upinzani wao uliokuwepo nchini Hispania na kuuleta England na Alonso alicheza chini ya makocha hao wote.
Alonso alizungumza na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher kuhusu utofauti wa mbinu kati ya Guardiola na Mourinho.
KUHUSU KUTUMIA VIUNGO:
Akitumia ubao wa kufundishia mbinu kwa wachezaji, Alonso ameeleza namna makocha hao wanavyotumia viungo ambapo amesema Mourinho anapenda viungo wawili wa kati, mmoja kila upande, wakati Guardiola anapenda mmoja kushuka chini zaidi kama alivyocheza wakati wa utawala wake Bayern Munich.
Malengo ya kumshusha mchezaji mmoja chini zaidi (kiungo mkabaji) na kuzuia mipira kufika safu ya ulinzi kwa urahisi ambapo wanatengeneza umbo la pembe tatu na walinzi wa kati.
Mbinu za Guardiola ni kushambulia zaidi, wakati Mourinho yeye ni kujilinda zaidi.
Usisome sana nilichokiandika hapa, tumwachie Xabi Alonso akuelekeza mwenyewe kwenye video hapo chini:
0 comments:
Post a Comment