Wednesday, September 7, 2016

Mabingwa wa Ulaya Ureno jana wameanza kampeni yao ya kusaka ushiriki wa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia vibaya baada ya kuchapwa mabao  2-0 dhidi ya Uswisi kwenye mchezo wa Kundi B uliofanyika kwenye Uwanja wa St. Jakob-Park jijini Basel nchini Uswisi.

Ureno, ambao waliingia uwanjani bila mpachika mabao wao mahiri na nahodha wao ambaye pia ni Mchezaji Bora wa Ulaya Cristiano Ronaldo kutokana na kuendelea na matibabu ya goti lake aliloumia mwezi Julai wakati Ureno ikiifunga Ufaransa katika Fainali ya EURO 2016, walijkuta wakipata kipigo hicho bila kikwao chochote.

Magoli hayo yalifungwa katika  kipindi cha kwanza mnamo dakika za 24 na 30 kupitia kwa Breel Embolo na Admir Mehmedi.

Katika mchezo huo, kiungo mpya wa Arsenal Granit Xhaka alitolewa nje dakika ya tisini baada ya kupata kadi mbili za njano zilizopelekea kulimwa kadi nyekundu

Katika Kund A, kulikuwa na mchezo mkali ambapo Sweden walikuwa wakiwakaribisha Uholanzi na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Goli la Sweden lilifungwa dakika ya 43 na Marcus Berg na Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi dakika ya 67.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video