Magoli yote ya Simba yalifungwa kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka suluhu dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Mechi hiyo iliwafanya Mzamiru Yassin Selemba na Shiza Ramadhan Kichuya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Waajiri wake wa Msimu uliopita, Mtibwa Suga, tangu wajiunge na Simba msimu huu wa dirisha la usajili.
Mohamed Ibrahim ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa lakini hakupata nafasi ya kucheza.
Kuna baadhi ya Dondoo kwa namba zilivutia kwenye mchezo huo kama alivyoripoti Mwandishi wa Tovuti ya shaffihdauda.co.tz , Dickson Masanja.
30 Namba kubwa zaidi ya jezi ilivaliwa na golikipa wa Mtibwa Sugar Abdallah Makangana.
10 Pointi ambazo Simba imefikisha baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa.
6 Pointi za Mtibwa baada ya kucheza mechi nne. Imeshinda mechi mbili na kupoteza michezo miwili.
9 Mtibwa wapo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi baada ya mchezo dhidi ya Simba.
2 Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC wanaoongoza ligi.
Katika mechi saba zilizopita, Mtibwa haijapata ushindi ushindi dhidi ya Simba. Imetoka sare kwenye mechi mbili na kupoteza mechi tano.
Rekodi za Simba vs Mtibwa Sugar
11/09/16 Simba 2-0 Mtibwa Sugar
15/05/16 Mtibwa Sugar 0-1 Simba
16/01/16 Simba 1-0 Mtibwa Sugar
14/03/15 Simba 1-0 Mtibwa Sugar
01/11/14 Mtibwa 1-1 Simba
05/02/14 Mtibwa Sugar 1-1 Simba
14/09/13 Simba 2-0 Mtibwa Sugar
0 comments:
Post a Comment