Arsène Wenger amekiri kwamba angepambana na na mahasimu wake Chelsea kumsajili Diego Costa mwaka 2014 kama angekuwa anafahamu kwamba mchezaji huyo alikuwa akipatikana, lakini akiwaonya wachezaji wake kuwa makini na kutoingia kwenye mtego wa starika huyo kuelekea mchezo wa leo.
Ndani ya michezo mitatu tu ya Premier League ambayo Costa amecheza dhidi ya Arsenal, ameshafunga magoli mawili na kusababisha kadi mbili nyekundu, na sasa Wenger anaamini kwamba wachezaji wake wanapaswa kuwa na umakini wa hali ya juu kupambana na mchezaji huyo
Katika mchezo wa kwanza Gabriel Paulista alipewa kadi nyekundu baada ya kudaiwa kumkanyaga kwa makusudi, huku nyingine ni ile aliyopewa Per Mertesacker baada ya kumchezea rafu wakati akienda kufunga.
“Tangu msimu umeanza ameonakana kubadilika na kuwa mtu mwema, amekuwa akitimiza majukumu yake zaidi na hali hiyo inamfanya kuwa hatari zaidi,” amesema Wenger,
Akaogeza: Halafu sikuwahi kujua kama angeondoka Atlético Madrid wakati ule, nilishangazwa sana.”
0 comments:
Post a Comment