Friday, September 23, 2016

Jose Mourinho ameripotiwa kutishia kuharibu uso wa Arsene Wenger kufuatia vita ya maneno kati ya wawili hao mwaka 2014.

Uhusiano mbaya wa Mourinho na Wenger ulirudi tena mwaka 2013 wakati Mourinho aliporejea Chelsea kwa mara huku kwa nyakati tofauti kila mmoja akirusha kijembe kwa mwenzake.

Ugomvi mkubwa wa kukumbukwa kati ya wawili hao ni pale Wenger alimrushia dongo Mourinho kwa kusema kwamba, kauli ya Mourinho juu ya Chelsea kuwa na nafasi finyu ya kuchukua ubingwa wa Premier League msimu wa 2013-14 ni kuogopa kufeli.

Kauli hiyo ilimpelekea Mourinho kutoa majibu ya dhihaka kwa Mfaransa huyo kwa kumwita "specialist in failure" yaani bingwa wa kufeli, wakati huohuo akionesha kukasirishwa na kauli aliyoitoa Wenger baada ya kuuzwa kwa Juan Mata kwenda Manchester United.

Hapo ndipo inapoelezwa kuwa Mourinho alitoa kauli hiyo lakini akiwa nje ya vyombo vya habari kwa kusema: "Siku moja nitamtafuta nje ya ulimwengu wa soka na kumpasua uso wake.'"

Tangu ajiunge na Manchester United, Mourinho bado hajakutana na Wenger huku wakitarajiwa kukutana Novemba 19 pale timu hizo zitakapokutana katika dimba la Old Trafford.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video