Wednesday, September 21, 2016


Victor Emenayo akiwa kwenye jezi ya Shahdagh Qusar FK

Udanganyifu wa umri kwa wachezaji hasa wa kutoka bara la Afrika limekuwa ni suala sugu sana hali inayopelekea wakati mwingine wachezaji hao kuumbuka pale uchunguzi thabiti unapochukuliwa.

Kumeibuka stori nyingine ya kuchekesha na kusikitisha huko nchini Azerbaijan juu ya mchezaji wa Kinigeria juu ya udanganyifu wa umri.

Mtu huyo anajulikana kwa jina la Victor Emenayo, ambaye anacheza kunako klabu ya Shahdagh Qusar FK.

Emenayo amekumbwa na shutuma hizo kutokana na umri wake na sura yake kuwa tofauti kabisa.

Kwa mujibu wa passport, Emenayo anaonekana kijana mwenye umri wa miaka 23.

Lakini klabu  hiyo ya Shahdagh Qusar FK anayocheza mchezaji huyo inadai kwamba umri sahihi wa Emenayo ni miaka zaidi ya 40 na sio 23 kama ilivyoandikwa kwenye passport yake.

Emenayo amekana kuongopa umri
Baada ya habari hiyo kuibuka, moja ya tovuti inayojulikana kwa jina la New Fanzone Blog imedai kuongea moja kwa moja na Victor Emenayo na kusema kwamba mchezaji huyo amekataa kabisa kuwa amedanganya umri.

Emenayo amesema: "Inakuaje mtu anatilia shaka umri wangu wa miaka 23 eti kwa kuangalia sura au mwonekano wangu. Mimi sio muongo.

Wengine wanadai kwamba inawezekana Emenayo anasumbuliwa na ugonjwa wa Lorde 'Lorde Disease', ambao huwafanya watu kuonekana wakubwa kuliko uhalisia wa umri wao. Hata hivyo, Emenayo ameshindwa kuthibitisha suala hilo.


Passport ya Victor Emenayo

Sakata lake linafanana na lile la Joseph Minala  raia wa Cameroon
Stori hii ya Victor Emenayo inakumbusha sakata la Joseph Minala aliyekuwa akicheza Lazio

Mwaka 2014, wengi walimshutumu Minala juu ya kudanganya umri wake. Minala alisema ana umri wa miaka 17, lakini uhalisia ulionesha kuwa ana umri wa miaka 42.

Joseph Minala

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video