Thursday, September 15, 2016

Shabiki mkubwa wa Manchester United Paddy Lawler aliyekuwa akisumbuliwa na mardhi ya saratani kwa muda mrefu hatimaye amefariki dakika 45 tu baada ya kuonana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Paddy, babu wa miaka 73 kutoka eneo la Wythenshawe, Manchester, aliiambia familia yake kwamba angepnda kuonana na baadhi ya wachezaji wa Mashetani Wekundu hao kabla ya kufikwa na umauti. 

Ili kukidhi matakwa ya babu huyo, mjukuu wake Kayleigh, 27, alipost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook kuujulisha umma kwamba yeyote ambaye angepata ujumbe huo awafikishie wachezaji wa Man United ili kutimiza ndoto za babu yake.

Posti hiyo ilishewa zaidi ya mara 1,000, kabla ya kumfikia mpwa wa winga wa United Jesse Lingaard.

Siku tatu baadaye baadhi ya wachezaji nyota wa United - Marcus Rashford, Jesse Lingard, Ashley Young na Timothy Fosu-Mensah waliamua kwenda kumtembelea babu huyo.

Punde tu baada ya kumwona mzee huyo, haikupita hata saa moja mzee akafariki dunia.

Kayleigh ametoa shukrani zake za dhati kwa wachezaji hao, na kuwaelezea kama "watu wenye moyo wa utu wa kipekee".

Ujumbe wake wa Facebook baada ya nyota hao kuja ulikuwa unasomeka hivi: "Iwafikie ninyi vijana bora wanne. Asanteni sana kwa msaada wenu. Nahisi sasa babu yangu atakuwa ameondoka na furaha."

Post yake ya awali kabla ya wachezaji hao kuja ilisomeka: "Tafadhali jamani kama kuna mtu anaweza kushea ujumbe huu kuwafikia japo wachezaji wachache tu wa Manchester United players ili waje kumtembelea babu yangu, siku moja tulimuuliza kitu gani angependa kufanyiwa kabla ya kufikwa na umauti na ndipo aliposema angependa kuonana na wachezaji wa United, sasa nimetuma email kwenye Taasisi ya Mufc (Mufc foundation), lakini sijajibiwa mpaka sasa!

"Na mpaka sasa sijafahamu amebakisha siku ngapi za kufariki na ningependa kumfanyia hili kama surprise, amekuwa ni mshabiki mkubwa sana na ningependa sana nifanikishe hili kwa babu yangu!

"Nafahamu fika kwamba atafurahi sana kama atafanikiwa kuwaona wachezaji hao

"Thankyou to u all Xxx"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video