David Ospina jana alikuwa mtu mwingine kabisa. Aliiokoa Arsenal kupoteza mchezo kwa asilimia 100 baada ya kuokoa hatari za waziwazi kabisa ziliokuwa zikipelekwa na PSG.
Kama si ubora wa Ospina basi Arsenal jana wangeweza kufungwa hata magoli manne na PSG, lakini uamkini wa hali ya juu wa mlinda lango huyo wa kimataifa wa Colombia ndiyo ulikuwa chachu ya sare ya bao 1-1 kati ya Arsenal na PSG.
Kabla ya mechi watu waliponda sana maamuzi ya Wenger kumuanzisha Ospina badala ya Petr Cech, lakini baada ya mechi wote walibadilika
Soma comments za watu hapo chini baada ya mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Parc des Princess.
0 comments:
Post a Comment