MESUT OZIL ameripotiwa kusaini mkataba mpya mnono ambao ndani yake kuna kipengele kinachosema apewe jezi namba 10.
Kulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya mustakabali wa Ozil klabuni hapo juu kuongeza mkataba mpya mbali na huu wa sasa unaoisha mwaka 2018.
Kwa mujibu wa jarida la Bild kutoka nchini Ujerumani, Ozil amesaini mkataba huo mnono ambao hata hivyo bado haujawekwa wazi
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ,27, awali alikuwa akilipwa paundi 140,000 kwa wiki lakini inaarifiwa kuwa mshahara wake umepanda zaidi baada ya kusaini mkataba mpya.
Ozil pia atapewa jezi namba 10 baada ya Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima.
Arsenal sasa wamebakiwa na mtihani mmoja tu wa kumbakisha Alexis Sanchez ambaye taarifa za awali zinadai kwamba mazungumzo yako mbioni kuanza.
Mkataba wa Sanchez wa sasa unatarajiwa kuisha mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment