- Katika jumla ya michezo yote 10 waliyokutana na Dortmund, Real Madrid wameshinda mara 4, sare mara 3 na wamefungwa mara 3.
- Katika michezo mitano waliyokutana na Real Madrid Signal Iduna Park, Dortmund hawajafungwa hata mchezo mmoja kati ya mitano, wameshinda mara 3 na kutoka sare mara 2.
- Mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni kwenye robo fainali ya Champions League msimu wa 2013/14. Real walishinda kwa wastani wa mabao 3-2 margin. Mchezo wa kwanza Dortmund walifungwa mabao 3-0 na wao kulipiza nyumbani kwa kushinda mabao 2-0.
- Real Madrid hawana rekodi nzuri kwa timu za Ujermani wakiwa ugenini kufuatia kufungwa magoli 2-0 na Wolfsburg kwenye robo fainali ya Champions League msimu uliopita. Hata hivyo Real walifuzu baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano.
0 comments:
Post a Comment