Friday, September 16, 2016

Ligi Kuu ya England inaendelea leo ambapo Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuwakaribisha Liverpool, mchezo utaofanyika saa 4:00 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Taarifa muhimu kutoka kila timu

Chelsea
David Luiz atakuwa akicheza kwa mara ya kwanza tangu arejee klabuni hapo kutoka PSG aliposajiliwa kwa ada ya paundi mil 34.

Luiz atapangwa mahsusi kuziba pengo la nahodha na beki mkongwe wa klabu hiyo John Terry, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyopata katika mchezo dhidi ya Swansea wikiendi iliyopita

Liverpool.
Beki waa Liverpool Dejan Lovren anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Leicester kutokana na kusumbuliwa na macho, ambapo Liverpool walishinda mabao 4-1 win.

Philippe Coutinho atajumuishwa kikosini leo baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na kupumzishwa kufuatia safari ndefu kutoka Brazil.

Kauli za mameneja
Kocha wa Chelsea Antonio Conte: "David Luiz atacheza kwa mara ya kwanza na tunaamini atafanya vizuri.

"Tunataraji atacheza vizuri, na kwa umakini mkubwa. Sote tunafahamu kwamba David ni mchezaji mzuri na tunajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha anakuwa katika hali nzuri ili kucheza katika kiwango bora.

"Nina imani naye kubwa sana. Ni mchezaji mzuri na nimeona mambo mazuri sana wakati akiwa mazoezini ."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp juu ya Diego Costa: "Ni mpambanaji wa ukweli akiwa uwanjani. Anautumia mwili wake kisawasawa na huo ndio ubora wake. Kwenye mchezo dhidi ya Swansea alionesha ubora wa hali ya juu.

"Ni mchezaji wa kiwango cha dunia na hicho ndicho mashabiki wa soka wanaweza kuongea juu ya Costa.

"Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Chelsea na sasa wamerudi kwenye mstari, hivyo tunahitaji kuwa makini kwelikweli."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video