Son Heung-min ameendelea kuwa kwenye kiwango bora baada ya kuipa Tottenham goli lililowapa ushindi wa kwanza kwenye Champions League dhidi ya CSKA Moscow.
Nyota huyo wa kimataifa wa South Korea amefunga bao lake la tano kwa Spurs msimu huu kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Erik Lamela.
Spurs walipoteza mchezo wao wa kwanza nyumbani walipofugwa bao 1-0 dhidi ya Monaco.
Spurs walisafiri bila ya nyota wake kadhaa kama Danny Rose, Eric Dier, Mousa Dembele, Moussa Sissoko na Harry Kane ambao woe kwa pamoja wanasumbuliwa na majeraha.
Dondoo muhimu
- Spurs wameshindwa kupata goli katika kipindi cha kwanza kwenye mechi tano kati ya sita zilizopita za Champions League.
- CSKA mapaka sasa wamesharuhusu goli kwenye kila mchezo kati ya 24 mfululizo iliyopita ya Champions League, wakiifikia rekodi ya Spartak Moscow (2000-2006).
- Son Heung-min (Spurs, Bayer Leverkusen) amekuwa mchezaji wa pili kutoka bara Asia baada ya Park Ji-sung (PSV, Manchester United) kuzifungia magoli timu tatu tofauti kwenye Champions League.
- Lacina Traore amekutana na Spurs mara nne akiwa na timu tofauti-tofauti- mara mbili akiwa na Monaco, mara moja na Anzhi Makhachkala na sasa akiwa CSKA (D1 L3). Ameshindwa kufunga mara zote alizokutana na Spurs.
0 comments:
Post a Comment