Thursday, September 8, 2016

Nyota wa zamani wa Arsenal Ray Parlour ameainisha kwamba, Diego Simeone ni kocha pekee ambaye Arsenal wanapaswa kumchukua endapo Wenger ataamua kustaafu.

Wenger, ambaye ndiye kocha mwenye muda mrefu zaidi kuliko makocha wote kwenye Ligi ya England mkataba wake na Arsenal unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu, na kama ataamua kuondoka klabuni hapo atakuwa ameitumikia  kwa miaka 20.

Kwa wiki kadhaa sasa Eddie Howe amekuwa akitajwa kama mrithi wa Wenger , lakini Parlour anahisi kwamba si sahihi kwa kocha huyo kijana mwenye asili ya England badala yake Simeone ndiye mtu sahihi kwa nafasi hiyo.

"Sidhani kama atakuwa akifahamu namna ya kuwavutia wachezaji wakubwa kutoka nje ya England," Parlour aliiambia talkSPORT.

"Ni kweli anafanya kazi nzuri sana kwenye klabu ya Bournemouth na anaweza kuwa kocha mzuri wa Arsenal kwa siku za baadaye, lakini naamini kwa sasa ni mapema mno kupewa jukumu hilo."

Parlour aliongeza: "Simeone, endapo ataamua kuondoka LaLiga, hilo hatujui, lakini naamini atakuwa na hamu ya kuonja ladha ya Premier League dhidi ya makocha kama Guardiola, Mourinho, Klopp na mameneja wengine kama hao.

"Atakuwa mtu sahihi kama atakuja Arsenal endapo wataamua kubadilisha kocha mwishoni mwa msimu."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video