TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba imepokea taarifa ya msiba ya Kocha wake wa zamani James Aggrey Siang'a kwa mshtuko na masikitiko makubwa sana.
Taarifa hiyo imeleta taharuki na majonzi sio kwa viongozi tu, bali kwa wanachama na washabiki wa klabu kote nchini.
Klabu kwa sasa inasubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia ya marehemu huko Bungoma nchini Kenya, kwa ajili ya kushiriki kwenye msiba na mazishi ya nguli huyu wa africa ya mashariki.
Kocha Siang'a anakumbukwa kwa mengi ndani ya Klabu,ikiwa ni pamoja na kuipa mataji kadhaa na pia kuiwezesha klabu kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika mwaka 2003.
Huu ni msiba mzito pia kwa wapenzi wa kandanda nchini,kwani kocha Siang'a alikuwa Mwalimu wa timu ya Taifa na ikumbukwe aliiwezesha timu ya taifa kufika fainali ya kombe la Challenge mwaka 2002 katika mashindano yaliyofanyika nchini.
Klabu itaomboleza msiba huu kwa wiki moja na inamuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu.
BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA,JINA LAKE LIHIDIMIWE
AMEEN.
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
0 comments:
Post a Comment