Tuesday, September 6, 2016

Mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazokuwa zikifanyika jijini Dar es Salaam sasa zitakuwa zikichezwa kwenye Uwanja wa Uhuru almaarufu Shamba la Bibi badala ya Uwanja wa Taifa, imeripotiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Licas, mchezo kesho kati ya Simba SC na Ruvu Shooting ndiyo utakuwa wa kwanza kuchezwa katika uwanja huo tangu ukabidhiwe rasmi.

“Napenda kuwafahamisha kuwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umeanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza,” Lucas amesema.

Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ambapo, jijini Dar es Salaam, Simba SC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting, Ndanda wakiwakaribisha Yanga mkoani Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kwingineko mkoani Mbeya katika Uwanja wa Sokoine, Wajelajela Tanzania Prisons watawakaribisha Wanalambalamba Azam FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video